Athari za Kikikuyu katika kujifunza kiswahili sanifu katika shule za upili Kaunti ndogo ya Othaya Kaunti ya Nyeri, Kenya

Show simple item record

dc.contributor.author Wanjala, Vincent
dc.contributor.author Oginga, Evans
dc.contributor.author Mwaura, Frevian
dc.date.accessioned 2023-10-26T14:10:16Z
dc.date.available 2023-10-26T14:10:16Z
dc.date.issued 2022
dc.identifier.uri https://ir.gretsauniversity.ac.ke/xmlui/handle/20.500.12736/3797
dc.description.abstract IKISIRI Watu wengi hukumbwa na matatizo kadha wanapojifundisha na wanapofundishwa lugha fulani hasa lugha ya pili katika Maisha yao. Matatizo haya husababisha changamoto katika maisha ya mhusika ikiwemo mawasiliano na elimu. Lengo kuu la utafiti huuni kubaini athari za lugha ya kikikuyu katika kujifunza lugha ya Kiswahili katika kaunti ndogo ya Othaya, kaunti ya Nyeri. Malengo ya utafiti huu ni; Kubaini namna kikikuyu kinavyoathiri uwezo wa wanafunzi wa kutumia upatanisho sahihi wa kisarufi katika sentensi katika shule za upili, kaunti ndogo ya Othaya, Nyeri Nchini Kenya, Kuweka wazi athari za kikikuyu kwa uwezo wa wanafunzi wa matumizi yafaayo ya msamiati katika shule za upili, kaunti ndogo ya Othaya, kaunti ya Nyeri, Nchini Kenya, Kubaini namna kikikuyu kinaathiri uwezo wa wanafunzi wa utamkaji ufaao wa sauti katika shule za upili, kaunti ndogo ya Othaya, kaunti ya Nyeri, nchini Kenya. Utafiti ulilenga jumla ya shule 34 zilizo na jumla ya wahojiwa 14,314. Mbinu za uteuzi wa sampuli wa mpangilio na uteuzi wa maksudi. Mbinu za ushiriki na insha zilitumiwa katika kukusanya data. Data zilichanganuliwa kwa kutumia mfumo wa tarakilishi wa kuchanganua data za kisayansi wa SPSS. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba lugha ya Kikuyu inaathiri uwezo wa wanafunzi kutumia upatanisho sahihi wa kisarufi, pia ilibainika kuwa wanafunzi waliokuwa wameathiriwa na lugha hii wanashindwa kutumia misamiati ya Kiswahili vilivyo. Zaidi, utafiti ulionyesha kuwa lugha ya kikuyu huathiri wazungumzaji wanafunzi wayo katika utamkaji wa sauti za Kiswahili sanifu. en_US
dc.publisher Gretsa University en_US
dc.subject Research Project en_US
dc.title Athari za Kikikuyu katika kujifunza kiswahili sanifu katika shule za upili Kaunti ndogo ya Othaya Kaunti ya Nyeri, Kenya en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search the Digital Repository


Browse

My Account