Abstract:
IKISIRI
Watu wengi hukumbwa na matatizo kadha wanapojifundisha na wanapofundishwa lugha fulani
hasa lugha ya pili katika Maisha yao. Matatizo haya husababisha changamoto katika maisha ya
mhusika ikiwemo mawasiliano na elimu. Lengo kuu la utafiti huuni kubaini athari za lugha ya
kikikuyu katika kujifunza lugha ya Kiswahili katika kaunti ndogo ya Othaya, kaunti ya Nyeri.
Malengo ya utafiti huu ni; Kubaini namna kikikuyu kinavyoathiri uwezo wa wanafunzi wa
kutumia upatanisho sahihi wa kisarufi katika sentensi katika shule za upili, kaunti ndogo ya
Othaya, Nyeri Nchini Kenya, Kuweka wazi athari za kikikuyu kwa uwezo wa wanafunzi wa
matumizi yafaayo ya msamiati katika shule za upili, kaunti ndogo ya Othaya, kaunti ya Nyeri,
Nchini Kenya, Kubaini namna kikikuyu kinaathiri uwezo wa wanafunzi wa utamkaji ufaao wa
sauti katika shule za upili, kaunti ndogo ya Othaya, kaunti ya Nyeri, nchini Kenya. Utafiti
ulilenga jumla ya shule 34 zilizo na jumla ya wahojiwa 14,314. Mbinu za uteuzi wa sampuli wa
mpangilio na uteuzi wa maksudi. Mbinu za ushiriki na insha zilitumiwa katika kukusanya data.
Data zilichanganuliwa kwa kutumia mfumo wa tarakilishi wa kuchanganua data za kisayansi wa
SPSS. Matokeo ya utafiti huu yalionyesha kwamba lugha ya Kikuyu inaathiri uwezo wa
wanafunzi kutumia upatanisho sahihi wa kisarufi, pia ilibainika kuwa wanafunzi waliokuwa
wameathiriwa na lugha hii wanashindwa kutumia misamiati ya Kiswahili vilivyo. Zaidi, utafiti
ulionyesha kuwa lugha ya kikuyu huathiri wazungumzaji wanafunzi wayo katika utamkaji wa
sauti za Kiswahili sanifu.